Tuesday 14 October 2014

Diamond Platnumz Afunguka Kiundani Juu ya Tetesi za Kuwa na Ugomvi na Ali kiba

Diamond na Alikiba ndio wasanii wa bongo fleva wenye timu mbili kubwa zamashabiki waliogawanyikana kuwashindanisha kwa niaba yao, Team Diamond v/s Team Alikiba, ushindani ambao umevalishwa ‘mask’ za ‘beef’ ambayo Nasib Abdulamedai kuwa haipo.Platnumz ambaye alikuwa bado hajaamua kuzungumzia tofauti hizo ameamua kufunguka juu ya ushindani pamoja na ‘beef’ iliyokuwa inazungumzwa baina yake na muimbaji huyo wa ‘Mwana’.“Nimekua nikiskia muda mrefu vimezungumziwa sana, kwenye mitandao katika nini, sijui kwanini vinazungumziwa hivyo” aliiambia 255 ya XXL ya Clouds Fm “Unajua kuna time ikifika inabidi uangalie na kuna vitu uvizoee tu sababu havikuanza leo hivi vitu siotu kwa Ali, ukiwa unafanya vizuri ni msanii yeyote ambaye atakuwepo nae anafanya nyimbo au akatoa nyimbo yaani utakuja utashindanishwa nae tu, atakuja huyu na huyu na huyu, lakini wewe mwenyewe tu kuangalia heshima yako iko wapi kuangalia kazi zako unazifanyaje ubora wake”.“Tangia mwanzo yaani inavyoanza ishagatokeaga hivyo ilikua sijui kwa Belle 9, ilitoka kwa Belle 9 ikaja nafikiri sijui Sam Wa Ukweli ilikua, ikaja sijui kwa Bob Junior, ikaja pia kwa Ali, ikatoka kwa Ali tena ikaja ikaondoka ikaenda kwa Omary I mean Ommy Dimpoz, ikatoka tena ikaja kwa Richard Mavoko, so kila time inavyokuwa inaenda unafanya vizuri hivyo vitu vinakua vinatokea, so ni we mwenyewe kuangalia na watu wasiokuwa na upeo wanaweza wakahisi hawa watu wana tatizo kumbe si tatizo ni vitu ambavyo vitakuwepo tu kwasababu mashabiki wana tabia wakiona mtu anafanya hichi na we unafanya kitu mkiwa katikakazi inayofanana hivyo vituvitatokea yaani watu watashindanisha, unaweza hata ukashindanishwa na mtu ambae hata hakufikii kiwango kabisa”.“Hata kwenye boxing ipo, ukiangalia hata kuna kipindi ilikuwa TMK na East Coast, ilikuwaga kwa Dully na T.I.D hivi ni vitu vya kikazi hata kwenye mpira ndio maana kuna Simba na Yanga, lakini haimaanishi Simba na Yanga ni maadui wakikutana Ngassa ntakupiga ngumi au flani ah ah..”Diamond amesema kuwa kama Alikiba alikuwa na tatizo na yeye anaamini angeweza kumfata na kumwambia sababu amefahamiana nae kabla hajakuwa mwanamuziki.“Sasa hivi yaani karibia mwaka wa tano, Mi tangia nianze kufanya muziki sijawahi kudrop kila siku nazidi kupanda juu…so hivyo vitu lazima vitatokea lazima nivikubali, inawezekana we unasema we unasema we hauna tatizo lakini mwenzio akawa anahisi wewe una tatizo nae, lakini naamini kama angekuwa anahisi kama mimi nina matatizo na yeye angenifata akaniambia kwa sababu mimi sijajuana na Ali kwenye muziki, nimejuana na Ali kabla sijakuwa mwanamuziki, nimemjua Ali kupitia dada yangu Queen Darleen so alikuwa an uwezo wa kunifata akaniambia personally kwamba bana umefanya hichi na hichi na hichi”.Diamond amemaliza kwa kusema kuwaomba media na mashabiki wasifanye ionekane kama wana beef binafsi bali wazishindanishe kazi ili kukuza muziki wa Tanzania.“Ukiniuliza mimi kiundani kabisa siamini kama kutakua na tatizo la damu ya mtu na mtu, bali ni vitu ambavyo vipo vya kisanaa au vya kimashabiki kwa mashabiki. Mi nasisitiza sana media na watu wasitengeneze kufanya kama ni matatizo ya mtu namtu kwasababu kisanaa inakua haijengi, lakini inapokuwa ni baina ya kazina kazi inakua inasaidia kwasababu inafanya watu wawe na changamoto ya kusema ngoja nitoe kazi kali ili nifanye kitu kizuri inasababisha muziki wetu ukue.”


Posted via mutashobya jr

No comments:

Post a Comment