KANDANDA

YANGA YAFANYA MAUAJI TAIFA: YAINYUKA JKT RUVU 5-1

Mrisho Ngasa (kulia) na Frank Domayo wakishangilia ushindi wa leo.

Didier Kavumbagu wa Yanga akijaribu kuwatoka wachezaji wa JKT Ruvu.
Yanga wakishangilia ushindi mnono wa leo dhidi ya JKT Ruvu.
Mashabiki wa Yanga wakiishangilia timu yao kwa nguvu.
Kikosi cha JKT Ruvu kilichoanza mtanange wa leo.
Kikosi cha Yanga kilichoiua JKT Ruvu.
TIMU ya Yanga imefanya mauaji baada ya kuishushia kipondo cha bao 5-1 timu ya JKT Ruvu katika mechi ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara iliyochezwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam hivi punde. Mabao ya Yanga yamewekwa kimiani na Mrisho Ngassa aliyefunga matatu 'hat trick' dakika ya 8, 15 na 49 wakati mengine yakifungwa na Didier Kavumbagu dakika ya 39 na Hussein Javu dakika ya 52 ya mchezo. Bao pekee la JKT Ruvu limewekwa kimiani na Idd Mbaga dakika ya 84.
Kikosi cha Young Africans
1. Deo Munish "Dida" - 30
2. Juma Abdul - 12
3. Oscar Joshua - 4
4. Nadir Haroub "Cannavaro" - 23
5. Mbuyu Twite - 6
6. Frank Domayo - 18
7. Saimon Msuva -27
8. Hassan Dilunga - 26
9. Didier Kavumbagu - 7
10. Mrisho Ngasa - 17
11. Hamisi Kizza - 20
Kikosi cha JKT Ruvu
1. Shabani Dihile
2. Damas Makwaya
3. Edward Charles
4. Omar Mtaki
5. Jamal Machelanga
6. Nashon Naftal
7. Sino Augustino
8. Emmanuel Swita
9. Idd Mbaga
10. Hussein Bunu
11. Kalaghe Mgunda
(PICHA ZOTE NA RICHARD BUKOS / GPL)

No comments:

Post a Comment